Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 36 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 324 2022-06-02

Name

Fatma Hassan Toufiq

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FATMA H. TOUFIQ aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itatunga Sheria ya Uanzishwaji wa Baraza la Taaluma kwa Kada ya Ustawi wa Jamii?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Fatma Hassan Toufiq, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na Uandaaji wa Sheria ya Taaluma ya Ustawi wa Jamii kwa kujumuisha maoni ya Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri na ya wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Chama cha Wataalam wa Ustawi wa Jamii Tanzania na itakapokamilika Muswada wa Sheria utawasilishwa Bungeni.