Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 37 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 332 | 2022-06-03 |
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza: -
Je, nyumba bora ya kuishi inatakiwa kuwa na sifa zipi na ni kwa nini Serikali haiweki ruzuku kwenye vifaa vya ujenzi?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naomba kumjibu Mheshimiwa Joseph George Kakunda, Mbunge wa Sikonge na Chifu wa Wakonongo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, nyumba ni mojawapo ya mahitaji muhimu ya mwanadamu. Nyumba bora ni ile yenye huduma bora kwa usalama na afya kwa wakazi wake. Jitihada za Serikali kuhakikisha nyumba bora zinajengwa kwa gharama nafuu ni pamoja na kuweka mazingira wezeshi ya uanzishwaji wa viwanda vya kuzalisha vifaa vya ujenzi, kufanya utafiti na kuwezesha matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kazi za ujenzi na kuhamasisha taasisi za fedha kutoa mikopo kwa ajili ya ujenzi, ukarabati na ununuzi wa nyumba.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved