Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 38 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 340 | 2022-06-06 |
Name
Fakharia Shomar Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. FAKHARIA SHOMAR KHAMIS aliuliza: -
Je, ni vijana wangapi wamepata nafasi za masomo nje ya nchi kwa mwaka 2015 - 2020 na kati yao ni wangapi wanatoka Zanzibar?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Fakharia Shomar Khamis, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimwa Naibu Spika, kwa mwaka 2015 - 2021, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar iliratibu ufadhili wa masomo katika Nchi za Uingereza, Hangaria, China, Morocco, Misri, Algeria, Urusi, Ujerumani, Msumbiji, Thailand, Mauritius, Iran na Indonesia. Watanzania walionufaika na ufadhili huo ni 856 ambapo kati yao wanaume ni 609 sawa na 71.1% na wanawake 247 sawa na 28.9%.
Mheshimwa Naibu Spika, nafasi za ufadhili wa masomo nje ya nchi hutolewa pasipo kujali mwombaji anatoka upande upi wa Muungano.
Mheshimwa Naibu Spika, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved