Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 40 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 356 2022-06-08

Name

Latifa Khamis Juwakali

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. LATIFA KHAMIS JUWAKALI aliuza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Bodi ya Mitaji kwa wahitimu wa elimu ya juu kama ilivyo kwa Bodi ya Mikopo ya wanafunzi wa Elimu ya Juu?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimwa Mwenyekiti, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa Latifa Khamis Juwakali, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilianzishwa mwaka 2004 ili kuweka utaratibu wa kisheria unaowawezesha wanafunzi wahitaji wenye sifa ya kujiunga na vyuo vikuu kumudu gharama za elimu ya juu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeupokea ushauri wa Mheshimiwa Mbunge, hata hivyo, Serikali imekuwa ikitoa mikopo kwa vijana kupitia halmashauri kwa kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani. Nashauri wahitimu wa elimu ya juu kutumia fursa hiyo kupata mitaji. Nakushukuru sana.