Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 3 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 39 | 2023-11-02 |
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE K.n.y. MHE. JULIANA D. MASABURI aliuliza:-
Je, lini Serikali itakipandisha hadhi Chuo cha Maendeleo ya Jamii Musoma ili kiweze kutoa shahada?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante na kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Didas Masaburi kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, ili chuo kiweze kufikia hatua ya kutoa elimu kwa ngazi ya shahada, kinatakiwa kiwe na ithibati kamili na kiwe na vigezo stahiki ikiwemo miundombinu ya kutosha kutoa kozi husika, rasilimaliwatu ya kutosha na yenye sifa stahiki na Bodi ya Uendeshaji.
Mheshimiwa Spika, sambamba na hatua zinazoendelea ili kuboresha mazingira ya chuo kwa ujumla wake, Wizara itaendelea kushirikiana na wadau wa kisekta kufanya tathmini ya kina kuhusu lini kozi hiyo ianze hasa kwa kuzingatia mahitaji halisi ya soko la ajira kwa wahitimu wa shahada, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved