Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 3 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 40 | 2023-11-02 |
Name
Michael Constantino Mwakamo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibaha Vijijini
Primary Question
MHE. MICHAEL C. MWAKAMO aliuliza:-
Je, lini Serikali itawasilisha Bungeni Muswada wa Sheria ya Wazee?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM, alijibu:-
Mheshmiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinisia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Michael Costantino, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, napenda kulithibitishia Bunge lako tukufu kuwa Serikali inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa wazee nchini. Sera ya Wazee ya mwaka 2003 iko katika hatua za mwisho za mapitio ili kujumuisha masuala mapya yanayojitokeza tangu kupitishwa kwa Sera hiyo iliyopo.
Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa mapitio ya Sera ya Wazee kutatoa fursa ya kutungwa Sheria ya Wazee na Serikali kuwakilisha Muswada huo wa Sheria ya Wazee Bungeni kwa hatua za sheria hiyo iliyotungwa, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved