Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 5 2023-10-31

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Jengo la Mama na Mtoto kwenye Kituo cha Afya – Loliondo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Loliondo ni moja ya Vituo vya Afya chakavu 199 vilivyoainishwa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa ajili ya upanuzi. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ukarabati pamoja na kuongeza miundombinu mbalimbali ikiwemo majengo ya Mama na Mtoto yenye uwezo wa kutoa huduma ya upasuaji wa dharura. Ahsante.