Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 47 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 412 2022-06-20

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itajenga Soko katika Mji Mdogo wa Chala Wilayani Nkasi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vincent Paul Mbogo, Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ipo katika hatua za awali za kupata eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 12,140 kwenye eneo la gulio lililopo katikati ya Mashete na Namanyere na ambalo litatosheleza mahitaji ya ujenzi wa soko katika Mji Mdogo wa Chala.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri itakapokamilisha taratibu zote za kupata eneo hilo na kuandaa andiko na gharama za mradi huo itatenga fedha kwenye bajeti ya mwaka 2023/2024 kwa ajili ya ujenzi wa soko hilo.