Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 11 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 180 2024-02-13

Name

Ally Juma Makoa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kondoa Mjini

Primary Question

MHE. ALLY J. MAKOA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaimarisha Mawasiliano ikiwemo Minara ya Simu na usikivu wa Radio ya Taifa (TBC) – Kondoa?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ally Juma Makoa, Mbunge wa Kondoa Mjini kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) wakishirikiana na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) imekamilisha ujenzi wa majengo ya mitambo ya redio pamoja na miundombinu ukiwemo mnara wa redio wilayani Kondoa ambapo kwa sasa TBC wanasubiria vifaa ambavyo vipo katika hatua ya manunuzi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itafanya tathmini katika jimbo la Kondoa Mjini na kuona maeneo yaliyobaki yenye changamoto za mawasiliano na kuviingiza vijiji husika katika orodha ya miradi itakayotekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha. (Makofi)