Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 69 2023-11-06

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:-

Je, Serikali inazingatia vigezo gani kugawa fedha za Mfuko wa Jimbo?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Omar Issa Kombo, Mbunge wa Jimbo la Wingwi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Jimbo umeanzishwa kwa mujibu wa Sheria Na. 16 ya mwaka 2009 kwa lengo la kuwawezesha Waheshimiwa Wabunge kuchochea maendeleo ya Jimbo. Aidha, vigezo vinavyotumika kugawa fedha za mfuko wa Jimbo ni pamoja na idadi ya watu Jimboni asilimia 45, mgao sawa kila Jimbo asilimia 25, kiwango cha umaskini asilimia 20 na ukubwa wa eneo asilimia10, ahsante.