Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 6 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 77 2023-11-06

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza

Je Serikali inampango gani wa kupandisha Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa kuwa Chuo Kikuu kamili?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa ni sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu vya Tanzania na Mwongozo kuhusu Vyuo Vikuu Tanzania uliotolewa na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania mwaka 2019.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa Serikali inaendelea kukiimarisha Chuo Kikuu Kishiriki cha Mkwawa kama Taasisi ya Elimu ya Juu chini ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa lengo la kukifanya kuwa Chuo Kikuu kinachojitegemea. Serikali itakipandisha hadhi kitakapokidhi taratibu tulizojiwekea kama nchi na kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.