Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 6 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 86 | 2023-11-06 |
Name
Iddi Kassim Iddi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Msalala
Primary Question
MHE. IDDI K. IDDI aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga minara ya simu katika Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA WIZARA YA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Iddi Kassim Iddi, Mbunge wa Jimbo la Msalala, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imepata mtoa huduma wa kufikisha huduma za mawasiliano katika Kata ya Ntobo yalipo Makao Makuu ya Halmashauri ya Msalala. Kampuni ya Simu ya Vodacom ndiyo ilishinda zabuni ya kujenga mnara huo kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali.
Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Vodacom inaendelea na hatua mbalimbali za utekelezaji wa ujenzi wa mnara huo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved