Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 14 | Sitting 11 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 184 | 2024-02-13 |
Name
Stanslaus Haroon Nyongo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Mashariki
Primary Question
MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza kununua pamba toka kwa wakulima pindi bei ya pamba inapoporomoka katika soko la dunia?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, biashara ya pamba nchini hufanyika kwa kuzingatia hali halisi ya soko ilivyo. Serikali imekuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa bei inayotolewa kwa wakulima inaakisi uhalisia wa bei katika soko la dunia kwa wakati huo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na kutokuwiana kati ya uzalishaji na mahitaji ya pamba duniani, bei ya pamba hupanda na kushuka kulingana na hali ya wakati huo. Mathalani, katika kipindi cha miaka mitano iliyopita bei ya pamba kwa ratili katika soko la dunia, kwa mfano kwa mwaka 2020, ilifikia Senti 50 za dola ya Marekani; na mwaka 2021 bei ilipanda hadi kufikia dola 1.5 kwa ratili. Mwaka 2023 hadi mwanzoni mwa mwaka 2024 bei ilikuwa wastani wa senti 84 za dola ya Marekani.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutambua athari ya mabadiliko ya bei kwa wakulima wa pamba nchini, Serikali ipo katika hatua za awali za uanzishaji wa Mfuko wa Kinga ya Bei (Price Stabilization Fund) utakaotumika kumfidia mkulima wakati bei inaposhuka kwa kiasi kitakachokubalika kwa mujibu wa Sheria ya kuanzishwa kwake.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved