Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 2 | Community Development, Gender and Children | Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge | 7 | 2023-11-01 |
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ANATROPIA L. THEONEST aliuliza: -
Je, Wanawake wangapi wamekuwa Wabunge wa Majimbo na Madiwani katika chaguzi tatu mfululizo zilizopita?
Name
Ummy Hamisi Nderiananga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE NA URATIBU (MHE. UMMY H. NDERIANANGA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Anatropia Lwehikila Theonest, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha kuanzia 2010 hadi 2020 zilifanyika chaguzi tatu katika ngazi ya Ubunge na Udiwani. Katika chaguzi hizo, jumla ya Wabunge Wanawake 73 walishinda chaguzi hizo na kuchaguliwa kuwa Wabunge wa Majimbo. Aidha, kwa upande wa Madiwani Jumla ya wanawake 654 waliweza kuchaguliwa na hivyo kuwa Madiwani katika Kata husika.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved