Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 10 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 153 2023-11-10

Name

Jafari Chege Wambura

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rorya

Primary Question

MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza:-

Je, lini Serikali itafanya maboresho ya Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Wambura, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, rasimu ya Sera ya Taifa ya mwaka 1995, Toleo la 2023 liliwasilishwa na kujadiliwa katika Mkutano wa Baraza la Mawaziri, tarehe 18 Agosti, 2023. Aidha, Wizara imekamirisha maboresho ya rasimu ya sera kwa kuzingatia maoni ya Baraza la Mawaziri.

Mheshimiwa Spika, hatua inayofuata ni rasimu hiyo ya sera kujadiliwa katika Mkutano wa Kazi wa Baraza la Mawaziri kwa tarehe itakayopangwa, ahsante.