Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 49 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 432 2022-06-22

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:-

Je, mafanikio gani yamepatikana kupitia mpango wa umeme jazilizi na lini Kituo cha kupooza umeme cha Uhuru kitafanya kazi?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nishati, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwaza Sitta, Mbunge wa Urambo, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Tabora una jumla ya vitongoji 122 vilivyonufaika na mradi wa umeme jazilizi (densification) ambapo kati ya hivyo, vitongoji 27 vipo katika Jimbo la Urambo. Mradi huu wa umeme jazilizi unatarajia kuunganisha umeme katika majengo, makazi, na shule 7,209 ambapo kati ya hayo, 1,722 yapo katika Jimbo la Urambo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Kupooza Umeme cha Uhuru kipo kwenye mradi wa kuunganisha umeme wa Gridi ya Taifa katika Mkoa wa Kigoma ambapo katika mradi huo, njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Kidahwe Mkoani Kigoma itajengwa. Mradi huo utahusisha pia ujenzi wa vituo vitatu vya kupooza umeme msongo wa kilovoti 132 kuja 33 vya Urambo, Nguruka na Kidahwe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mradi wa Kuimarisha Gridi ya Taifa (The National Grid Stabilization Projects) imetenga jumla ya Shilingi bilioni 24 katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwa ajili ya kujenga njia ya kusafirisha umeme msongo wa kilovoti 132 kutoka Tabora hadi Urambo yenye urefu wa kilometa 115, na kukamilisha kituo cha kupooza umeme cha Urambo kilichoko Uhuru. Hivyo, kituo cha Kupooza Umeme cha Uhuru kitaanza kufanya kazi mwezi Juni, 2023 ambapo inatarajiwa kuwa ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tabora hadi Urambo itakuwa imekamilika, nashukuru.