Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 49 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo | 434 | 2022-06-22 |
Name
Mohammed Said Issa
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Konde
Primary Question
MHE. MOHAMED SAID ISSA aliuliza:-
Je, Serikali inaisaidiaje Zanzibar kupata faida ambazo TFF inazipata katika kuendeleza soka la Tanzania?
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TFF imeendelea kuhakikisha kuwa Zanzibar inanufaika na fedha za misaada kutoka FIFA ambapo hadi sasa miradi kadhaa ya kuendeleza soka imetekelezwa ikiwa ni pamoja na kusaidia timu za Taifa, mashindano ya ndani, mawasiliano na mafunzo kwa wadau wa michezo. Hata hivyo, Serikali inatambua changamoto zilizopo baina ya TFF na ZFF katika uendeshaji soka katika Taifa letu.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kutatua changamoto hizi, Wizara yetu pamoja na Wizara ya Michezo na Vijana Zanzibar zimeitisha kikao maalumu baina ya ZFF na TFF kwa lengo la kutatua changamoto hizo.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved