Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 49 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 436 | 2022-06-22 |
Name
Leah Jeremiah Komanya
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Meatu
Primary Question
MHE. LEAH J. KOMANYA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Mheshimiwa Leah Jeremiah Komanya, Mbunge wa Jimbo la Meatu, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kutekeleza Mpango wa Ujenzi wa Vyuo vya VETA kwa awamu katika mikoa na wilaya mbalimbali kulingana na upatikanaji wa fedha. Katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Meatu, wananchi wa Meatu wanashauriwa kutumia Vyuo vingine vya VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo kwa ajili ya kupata elimu ya mafunzo ya ufundi, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved