Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 7 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 100 | 2023-11-07 |
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itapeleka huduma ya mawasiliano ya simu Kata ya Masaka – Kalenga?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jackson Gedion Kiswaga, Mbunge wa Jimbo la Kalenga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) iliingiza Kata ya Masaka katika zabuni ya kufika huduma ya mawasiliano Vijijini kupitia Mradi wa Tanzania ya Kiditali, ambapo Kampuni ya Simu ya Vodacom ilishinda zabuni hiyo ya kufikisha huduma hiyo katika Kata ya Masaka yenye Vijiji vya Kaning’ombe, Saadani pamoja na Makota. Mpaka sasa Vodacom inaendelea na hatua mbalimbali za utekelezaji katika ujenzi wa mnara huo.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved