Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 2 | Planning and Investment | Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji | 21 | 2024-04-03 |
Name
Toufiq Salim Turky
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpendae
Primary Question
MHE. TOUFIQ SALIM TURKY aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga majengo ya viwanda kuwapangishia wawekezaji wazawa ili kuongeza idadi kwani gharama za kuanzisha kiwanda ziko juu?
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, mwelekeo wa Sera za Serikali katika uwekezaji ni kushirikiana kati ya sekta ya umma na sekta binafsi katika maendeleo ya viwanda. Serikali ina jukumu la msingi la kutwaa, kupima na kupanga matumizi ya ardhi, wakati sekta binafsi hukaribishwa na kuhamasishwa kuwekeza katika ujenzi wa miundombinu ya viwanda. Utaratibu huu umeshaanza kuzaa matunda ambapo hadi kufikia Desemba jumla ya kongani kubwa tatu za viwanda zimejengwa kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved