Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 14 | Sitting 4 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 55 | 2024-02-02 |
Name
Omar Issa Kombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wingwi
Primary Question
MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itatatua changamoto ya mawasiliano ya simu Micheweni, vijiji vya Sizini, Dodeani, Michungani, Mapofu, Msuka na Makangale?
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolijia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omar Issa Kombo, Mbunge wa Jimbo la Wingwi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Sizini kipo katika mradi wa awamu ya sita ambapo mnara katika kijiji hicho unajengwa na mtoa huduma ambaye ni Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL). Mnara huo upo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ambapo utakamilika na kuwashwa ifikapo Aprili, 2024. Aidha, Serikali imetekeleza ujenzi wa mnara katika kijiji cha Dodeani kupitia mradi wa awamu ya nne ya UCSAF ambapo mnara ulijengwa katika Shule ya Dodeani.
Mheshimiwa Spika, Aidha, Serikali itavifanyia tathmini vijiji vya Michungani, Mapofu, Msuka na Makangale kuangalia mahitaji halisi ili kuvifikishia huduma ya mawasiliano.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved