Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 12 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 194 2024-02-14

Name

Martha Festo Mariki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARTHA F. MARIKI aliuliza:-

Je, lini Serikali itatekeleza ahadi ya ujenzi wa Shule ya Sayansi ya Wasichana Mkoani Katavi?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Martha Festo Mariki, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa shule ya bweni ya wasichana kwa ajili ya masomo ya sayansi katika Mkoa wa Katavi unafanyika katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo katika Kata ya Katalala ambapo hadi sasa ujenzi upo asilimia 80. Shule hii imesajiliwa na kuandikisha wanafunzi 100 wa kidato cha kwanza mwaka 2024.