Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 1 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 13 2024-01-30

Name

Dr. Faustine Engelbert Ndugulile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigamboni

Primary Question

MHE. DKT. FAUSTINE E. NDUGULILE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kuendeleza eneo la ekari 1,000 lililotengwa kwa matumizi ya viwanda Kata ya Pembamnazi?

Name

Jerry William Silaa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ukonga

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, eneo la Pembamnazi lipo Manispaa ya Kigamboni na lina ukubwa wa ekari 1,000. Eneo hilo limetengwa kama hazina ya ardhi kwa ajili ya uwekezaji.

Mheshimiwa Spika, Wizara kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali inaendelea kutafuta wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kuwekeza katika eneo hilo. Hivyo, wawekezaji wenye nia ya kuwekeza katika maeneo hayo wawasilishe maombi yao Ofisi ya Ardhi Mkoa wa Dar es Salaam au kwenye mamlaka za uwekezaji wakiainisha kiasi cha ardhi wanachoomba na uwekezaji tarajiwa. Aidha, Wizara iko tayari kupokea ushauri Mheshimiwa Mbunge kuhusu uwekezaji katika eneo hilo. Ahsante.