Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 14 | Sitting 1 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 15 | 2024-01-30 |
Name
Juliana Didas Masaburi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KWAGILWA R. NHAMANILO K.n.y MHE. JULIANA D. MASABURI aliuliza:-
Je, Serikali haioni haja ya kusimamia sheria kikamilifu na kukomesha utaratibu wa wapangishaji nyumba kutoza pango kwa fedha za kigeni?
Name
Jerry William Silaa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukonga
Answer
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, kwa sasa hakuna sheria mahsusi inayoelekeza aina ya fedha inayotakiwa kutumika katika kutoza pango kwa wapangishaji wa nyumba. Hata hivyo, Benki Kuu imekuwa ikitoa miongozo kuhusu matumizi ya fedha za kigeni nchini ambayo pamoja na mambo mengine inakataza matumizi ya fedha za kigeni kwa wakazi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kulipia bidhaa na huduma nchini. Mwongozo unaotumika sasa ulitolewa mwezi Desemba, 2017.
Mheshimiwa Spika, ili kuboresha utendaji wa soko la nyumba nchini, Wizara ipo katika mchakato wa kutunga Sheria ya Milki ambayo pamoja na masuala mengine itaweka utaratibu wa utozaji wa pango hususan kwa raia wa Tanzania. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved