Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 13 | Sitting 4 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 114 | 2023-11-08 |
Name
Yahaya Omary Massare
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Manyoni Magharibi
Primary Question
MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza: -
Je, lini Tume ya Umwagiliaji itatimiza ahadi yake ya kuvuna maji ya mvua katika Mbuga inayozunguka Mji wa Itigi ili kuepusha mafuriko?
Name
Anthony Peter Mavunde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Dodoma mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Jimbo la Manyoni Magharibi, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu spika, katika Mwaka wa Fedha 2023/24, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya imetenga fedha kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kuweza kuchimba na kujenga mifereji ya kuongoza maji kutoka bonde linalozunguka Mji wa Itigi na kuelekeza maji hayo mashambani.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, utekelezaji wa ujenzi wa mifereji hiyo utasaidia kuepusha mafuriko yanayojitokeza katika Mji wa Itigi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved