Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 5 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 67 2024-02-05

Name

Bonnah Ladislaus Kamoli

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Segerea

Primary Question

MHE. BONNAH L. KAMOLI aliuliza:-

Je, lini kanuni mpya za malipo ya pensheni kwa wastaafu ya kila mwezi ya kutoka asilimia 50 mpaka 67 zitaanza kutumika?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCHAL P. KATAMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bonnah Ladislaus Kamoli, Mbunge wa Segerea, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa Serikali kupitia Gazeti la Serikali Na. 357 la tarehe 20 Mei, 2022 lilitangaza Kanuni Mpya ya Mafao ambayo iliboresha kiwango cha mafao ya pensheni ya kila mwezi kwa wastaafu kutoka asilimia 50 iliyokuwa ikilipwa awali na kuwa asilimia 67. Matumizi ya Kanuni hizo yalianza kutumika rasmi tarehe 1 Julai, 2022.

Mheshimiwa Naibu Spika, kanuni hizo ziliandaliwa kwa kushirikisha wadau wote muhimu (wadau upande wa Serikali, Wafanyakazi na Waajiri) kwa lengo la kufanya maboresho ya Pensheni ili kuyaainisha mafao ya wanachama na kuifanya mifuko kuwa endelevu, ahsante.