Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 5 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 75 2024-02-05

Name

Salim Mussa Omar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Gando

Primary Question

MHE. SALIM MUSSA OMAR aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuzuia wimbi kubwa la wasichana wenye umri chini ya miaka 18 kwenda klabu za usiku kwenye miziki na starehe?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mussa Omar Salim, Mbunge wa Gando, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inasimamia utekelezaji wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya mwaka 2009 kifungu cha 158(1)(b) ambacho kinakataza watoto wenye umri chini ya miaka 18 kushiriki shughuli za mikusanyiko ya usiku zikiwemo klabu na kumbi za starehe.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali inaendelea kutoa elimu ya malezi na makuzi ya watoto ili kuwapa wazazi na walezi uelewa wa athari za kuwaacha watoto bila ulinzi hasa wakati wa usiku na kuwakumbusha wajibu wao wa kulea na kutunza watoto katika maadili.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na hayo, tunaendelea kushirikiana na Wizara za Kisekta na wadau wa maendeleo hususan wamiliki wa kumbi za starehe, kwa lengo la kuweka mikakati na mbinu jumuishi za kusimamia ulinzi na usalama wa mtoto, ahsante.