Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 6 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 66 2024-04-15

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Bwalo katika Sekondari ya Malagarasi - Muhambwe lililosimama tangu mwaka 2017?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Mwaka wa Fedha 2016/2017, Serikali ilitoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa Bwalo la Chakula katika Shule ya Sekondari Malagarasi. Fedha hiyo ilitumika kukamilisha kazi za ujenzi wa bwalo na hadi sasa lipo katika hatua za umaliziaji.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua kuwa baadhi ya miundombinu ya bwalo hilo haijakamilika kujengwa. Hivyo, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga bajeti ya shilingi milioni 187 kwa ajili ya kuendelea na ukamilishaji wa ujenzi wa Bwalo katika Shule ya Sekondari Malagarasi.