Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 6 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 74 | 2024-04-15 |
Name
Joseph George Kakunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Sikonge
Primary Question
MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:-
Je, lini Serikali itasimamia ushushaji wa bei ya mbegu za mahindi kwa wakulima?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Kakunda, Mbuge wa Sikonge, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kusimamia udhibiti wa upandishaji holela wa bei za mbegu za mazao ya kilimo hususani mahindi kuanzia Mwaka wa Fedha wa 2023/2024, Wizara ya Kilimo imefanya yafuatayo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, moja, kupitia Taasisi ya TOSCI imechukua hatua za kutangaza bei elekezi ya mbegu za mahindi kwa reja reja na jumla ili kudhibiti upandishaji holela wa bei za mbegu. Pili, imeunda timu ya Wataalamu kutoka Wizara ya Kilimo, Taasisi ya TARI, ASA na TOSCI pamoja na sekta binafsi na inaongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Maendeleo ya Mazao. Pamoja na mambo mengine itaandaa mjengeko wa bei za mbegu za mazao ya kilimo kwa ajili ya bei elekezi zitakazokuwa zinatangazwa mwezi Septemba kila mwaka.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo imeyaandikia makampuni yote ya mbegu kuwasilisha taarifa za gharama za uzalishaji wa aina mbalimbali za mbegu ili kuimarisha utaratibu wa kupanga bei elekezi. Naomba nafasi hii kupitia Bunge lako Tukufu kuyakumbusha makampuni yote ya mbegu kuwasilisha taarifa hizo kabla ya tarehe 30 Aprili. Wizara haitasita kuyafutia leseni makapuni yote ya mbegu ambayo hayatawasilisha taarifa hizo kama zinavyohitajika.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inaendelea kuishirikisha sekta binafsi kutumia Ardhi ya ASA na TARI kuzalisha mbegu kwa utaratibu wa kuingia mikataba ya muda mrefu ili kuongeza upatikanaji wa mbegu kwa wakulima na kwa bei nafuu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved