Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 14 | Sitting 5 | Home Affairs | Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi | 78 | 2024-02-05 |
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER N. MATIKO aliuliza:-
Je, nini kinasababisha tofauti ya maslahi kati ya Askari wa Jeshi la Polisi na Askari wa Jeshi la Magereza?
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Esther Nicholas Matiko, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, maslahi ya Jeshi la Polisi na Jeshi la Magereza yanafanana kwa mujibu wa taratibu za Utumishi wa Umma na kama ilivyofafanuliwa kwenye sheria zilizoanzisha majeshi haya (Sheria Na. 1 ya mwaka 1939, Sura ya 322 na Sheria Na. 34 ya mwaka 1967 Sura ya 58 iliyorejewa mwaka 2002). Maslahi hayo ni pamoja na kupatiwa na kuboreshewa makazi, vitendea kazi, mishahara na posho, sare za kazi, ofisi na vituo vya kutolea huduma, udhibiti wa nidhamu pamoja na utoaji adhabu, utoaji na upandishaji wa vyeo, nashukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved