Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 5 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 79 2024-02-05

Name

Ali Juma Mohamed

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shaurimoyo

Primary Question

MHE. ALI JUMA MOHAMED aliuliza:-

Je, kuna mkakati gani wa kudhibiti ajali za bodaboda zinazogharimu maisha ya wananchi wengi?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ali Juma Mohamed, Mbunge wa Shaurimoyo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mikakati inayotumiwa na Serikali kupitia Jeshi la Polisi ili kudhibiti ajali za bodaboda ni pamoja na kutoa elimu juu ya matumizi bora ya barabara pamoja na uendeshaji vyombo vya moto kwa waendesha bodaboda kwa kushirikisha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), Mashirika ya Bima, Taasisi na Makampuni binafsi kama Bet Power, Ammend, Mabalozi wa Usalama Barabarani (RSA), Kiwanda cha Bia cha Serengeti, shule na vyuo vya udereva. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati mwingine ni kuchukua hatua za kisheria dhidi ya madereva wa vyombo vya moto wanaovunja sheria ya usalama barabarani pamoja na kushirikiana na TAMISEMI kuunda vikundi vya waendesha bodaboda ili kuhamasisha na kuheshimu sheria za usalama barabarani, ahsante. (Makofi)