Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2000-2005 Session 14 Sitting 13 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 220 2024-02-15

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buyungu

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza:-

Je, lini Skimu za Umwagiliaji za Katengera, Muhwazi, Gwanumbu na Ruhwiti katika Wilaya ya Kakonko zitakarabatiwa?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aloyce John Kamamba, Mbunge wa Jimbo la Buyungu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Bonde la Buyungu linalojumuisha Skimu za Katengera, Muhwazi, Ruhwiti, Ruhuru, Mgunzu, Kayonza, Lukoyoyo, Chulanzo, Asante Nyerere na Kilimo Kwanza. Kazi za upembuzi yakinifu na usanifu zinatarajiwa kukamilika mwezi Mei, 2024. Kukamilika kwa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika skimu hizi kutawezesha kupatikana kwa gharama halisi za ujenzi na ukarabati, hivyo kuwekwa kwenye mpango wa ujenzi na bajeti.

Mheshimiwa Spika, Mradi wa Umwagiliaji Gwanumbu umeendelezwa kwa kujengewa mfereji mkuu. Mradi huu unahitaji kufanyiwa usanifu wa miundombinu ambayo haijakamilika. Katika mwaka wa fedha 2024/2025 mradi wa umwagiliaji Gwanumbu utaingizwa kwenye mpango wa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kujua gharama halisi za ukarabati kabla ya kuingizwa kwenye mpango wa ujenzi na bajeti.