Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 13 Defence and National Service Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga taifa 224 2024-02-15

Name

Cecil David Mwambe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ndanda

Primary Question

MHE. CECIL D. MWAMBE aliuliza:-

Je, kweli kuna wazee wanaodai haki zao kutokana na ushiriki wao kwenye Vita vya Dunia au Jeshi la KAR?

Name

Dr. Stergomena Lawrence Tax

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nominated

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI K.n.y. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cecil David Mwambe, Mbunge Ndanda, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba wapo wazee waliopigana Vita ya Pili ya Dunia (1939 - 1945) wakiwa askari wa Jeshi la KING’S AFRICAN RIFLES (KAR) lililokuwa chini ya Serikali ya Kikoloni ya Uingereza. Haki wanazodai zinahusiana na mali walizoachiwa na Serikali ya Uingereza mara baada ya utawala wao Tanganyika kukoma.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.