Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 11 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 143 2024-04-22

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza uzalishaji wa zao la pareto nchini?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Kilimo imeendelea kutekeleza mikakati mbalimbali ya kuongeza uzalishaji wa zao la pareto. Mikakati hiyo ni pamoja na utafiti na uzalishaji wa mbegu bora, elimu ya kilimo bora na kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya kuongeza thamani na mashamba makubwa ya kilimo cha pareto.

Mheshimiwa Spika, kutokana na mikakati hiyo, uzalishaji wa pareto umeongezeka kutoka tani 3,150 mwaka 2022/2023 hadi tani 4,238 mwaka 2023/2024 sawa na ongezeko la 121% ya lengo la kuzalisha tani 3,500. Aidha, kilo 5,130 za mbegu bora za pareto zimesambazwa katika msimu wa 2023/2024 kwa wakulima 10,260 wa pareto katika mikoa sita inayolima zao hilo ambayo ni Mbeya, Iringa, Songwe, Njombe, Manyara na Arusha sambamba na mafunzo ya kilimo bora kwa wakulima 2,530.

Mheshimiwa Spika, viwanda vya kuchakata maua ya pareto vimeongezeka kutoka viwanda viwili vilivyokuwepo mwaka 2020/2021 hadi viwanda vinane mwaka 2022/2023 vinavyowezesha uongezaji wa thamani na kupanua wigo wa masoko ya pareto na bidhaa zake. Vilevile Serikali imeanza kushirikiana na Kampuni ya Pareto Tanzania (PCT) kuanzisha shamba la ekari 300 katika Wilaya ya Makete kama sehemu ya utekelezaji wa mpango wa kuanzisha mashamba makubwa, na mpango huo utaendelea katika maeneo mengine ya uzalishaji wa pareto.