Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 11 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 147 2024-04-22

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kufuta ada za Vyuo vya Ufundi hususani VETA?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa upatikanaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa vijana wengi wa Kitanzania katika maeneo yao kwa lengo la kuwawezesha kupata ujuzi utakaowawezesha au kuwasaidia kujiajiri au kuajiriwa.

Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha hilo, Serikali imekuwa ikitoa ruzuku ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi ili kuhakikisha kuwa Watanzania wanaotamani kupata mafunzo haya, wanayapata kwa gharama nafuu. Kwa sasa mwanafunzi wa bweni analipa ada ya shilingi 120,000 badala ya gharama halisi ya shilingi 860,000 wakati mwanafunzi wa kutwa analipa ada ya shilingi 60,000 badala ya shilingi 300,000.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kupunguza gharama za upatikanaji wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa kadiri uchumi wa nchi na mapato ya Serikali yatakavyoendelea kuimarika. Nakushukuru.