Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 52 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 457 2022-06-27

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. RITTA E. KABATI aliuliza: -

Je, ni lini Serikali italeta Bungeni mabadiliko ya Sheria ya Hakimiliki ili iwezeshe Mkataba wa Marakesh kutekelezeka kwa mujibu wa Sheria?

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Daktari Ritta Kabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Marekebisho ya Sheria tajwa yalishaletwa Bungeni na kupitishwa tarehe 7 Feburari, 2022. Kwa sasa Serikali ipo katika utaratibu wa kuandaa Kanuni za kusimamia Mamlaka ya usimamizi na kuiwezesha kibajeti kwa lengo la kuhakikisha wanufaika wa Mkataba huu wa Marsakesh wanapata machapisho mbalimbali watakayohitaji katika upataji wa Elimu na Habari ikiwa ni pamoja na kudhibiti machapisho ambayo yatakua kinyume na utaratibu na sheria za nchi. Ahsante.