Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 52 | Information, Culture, Arts and Sports | Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo | 458 | 2022-06-27 |
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Primary Question
MHE. HAMISI M. MWINJUMA aliuliza:
Je, kuna mpango gani kuruhusu watu/taasisi binafsi hasa za wasanii kukusanya mirabaha maeneo ya wazi yanayotumia kazi za sanaa?
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:
Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Hamisi Mohamed Mwinjuma, Mbunge wa Muheza, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali ina mpango wa kuruhusu watu binafsi na Taasisi kuanza kukusanya mirabaha na tayari mapendekezo yameshaletwa kwenye Financial Bill ya mwaka 2022. Aidha, inapendekezwa COSOTA kubaki na jukumu la kusimamia Hakimiliki na jukumu la ukusanyaji na ugawaji wa Mirabaha kwenda kwa Taasisi au Wadau binafsi yanii Collective Management Organizations (CMOs). Nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved