Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 43 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 551 2024-06-07

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza: -

Je, kuna mkakati gani wa kukarabati majengo yaliyojengwa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu Msingi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2022/2023 Ofisi ya Rais, TAMISEMI ilifanya tathimini ya mahitaji na hali ya miundombinu ya shule zote za msingi zikiwemo shule zenye majengo yaliyojengwa chini ya mpango wa maendeleo ya elimu msingi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuanzia mwaka 2022/2023 hadi 2023/2024 Serikali imekuwa ikitoa fedha kwa ajili ya ukarabati ambapo shilingi bilioni 70.39 zimetolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule 793.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha za ukarabati wa shule chakavu zikiwemo shule zenye majengo yaliyojengwa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu Msingi kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha.