Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 43 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 552 2024-06-07

Name

Rose Cyprian Tweve

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ROSE C. TWEVE aliuliza: -

Je, Halmashauri ngapi zimetekeleza agizo la Waziri Mkuu kununua dawa za viuadudu kutoka Kiwanda cha Kibaha ili kutokomeza mazalia ya mbu?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Rais, TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Afya kupitia Mpango wa Taifa wa kudhibiti Malaria imeendelea kusimamia na kuratibu utekelezaji wa afua ya unyunyuziaji wa viuadudu katika mazalia ya mbu yaliyotambuliwa katika halmashauri.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuzielekeza halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya kununua dawa za viuadudu. Aidha, katika mwaka wa fedha 2023/2024 jumla ya halmashauri 126 zimetenga shilingi milioni 775.89 kwa ajili ya ununuzi wa dawa hizo.