Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 180 2024-04-25

Name

Ally Anyigulile Jumbe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza:-

Je, vikwazo gani vinasababisha Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela usipandishwe hadhi kuwa Halmashauri ya Mji?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua mahitaji na umuhimu wa kuanzisha maeneo ya kiutawala ili kusogeza huduma karibu na wananchi. Aidha, uanzishaji wa maeneo ya utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa hufanyika kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya), Sura 287 na (Mamlaka za Miji), Sura 288 pamoja na Mwongozo wa Uanzishwaji wa Maeneo ya Utawala wa mwaka 2014.

Mheshimiwa Spika, Mamlaka ya Mji Mdogo wa Kyela ilianzishwa mwaka 2008. Serikali itakapoanza utekelezaji wa kuanzisha maeneo mapya ya kiutawala itaifanyia tathmini mamlaka hiyo na kuendelea na hatua za kuipandisha hadhi ikiwa itakidhi vigezo.