Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 42 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 544 2024-06-06

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI K.n.y. MHE. HUSSEIN N. AMAR aliuliza:-

Je, ni lini Vituo vya Afya Kharumwa na Nyang’hwale vitapatiwa X–Ray?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 hadi 2023/2024 jumla ya mashine 280 za kidijitali za x-ray na mashine za ultrasound 322 zimenunuliwa na kusimikwa katika vituo vya kutolea huduma za afya ya msingi. Aidha, Halmashauri ya Wilaya ya Nyang’hwale ilipokea mashine mbili za x-ray ambazo zimefungwa katika Hospitali ya Wilaya mwezi novemba, 2022.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuboresha miundombinu ya kutolea huduma za mionzi katika vituo vya kutolea huduma za afya vikiwemo Vituo vya Afya vya Kharumwa na Nyang’hwale.