Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 42 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 548 | 2024-06-06 |
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza:-
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa Kituo cha Utalii Kihesa, Kilolo chini ya mradi wa REGROW?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Spika, mnamo tarehe 26 Januari, 2024 Wizara ya Maliasili na Utalii ilisaini mkataba kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utalii katika eneo la Kihesa Kilolo, Mkoani Iringa kupitia Mradi wa REGROW. Aidha, tarehe 27 Januari, 2024 mkandarasi alikabidhiwa eneo la ujenzi na kuanza kazi. Mkataba huo ni wa miezi 12 na unatarajiwa kukamilika mwezi Januari, 2025. Hadi kufikia mwezi Mei, 2024 ujenzi wa jengo hilo umefikia 15% na ujenzi unaendelea.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved