Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 42 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 549 | 2024-06-06 |
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Kaskazini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-
Je, kuna mpango gani kuvipatia mawasiliano ya simu vijiji 13 na Kata za Mughunga, Ngimu, Makuro, Mudida, Ughandi, Msisi, Msange na Mgori?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa Kata za Ngimu, Kijiji cha Lamba, Kata ya Msisi Vijiji vya Mnung’una na Mkwae, Kata ya Msange, Vijiji vya Muriga na Endeshi UCSAF imeingia makubaliano na TTCL kupeleka huduma za mawasiliano katika kata tajwa. Aidha, UCSAF pia imeingia makubaliano na Vodacom kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano katika Kata ya Ughandi, Kijiji cha Misinko na kwa upande wa Kata ya Mudida, Kijiji cha Migugu UCSAF imeingia makubaliano na Kampuni ya Simu ya Halotel.
Mheshimiwa Spika, baada ya kukamilika kwa miradi hii, Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini ya hali ya mawasiliano katika kata hizo na kuchukua hatua stahiki kulingana na upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved