Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 46 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 599 2024-06-12

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Chuo cha VETA Wilayani Kyerwa?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa sasa inaendelea na utekelezaji wa azma ya kujenga chuo cha ufundi stadi katika kila mkoa na wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga vyuo vya ufundi stadi katika wilaya 64 kwa wilaya ambazo zilikuwa hazijajengewa vyuo vya ufundi stadi, pamoja na Chuo cha Mkoa wa Songwe. Aidha, Wilaya ya Kyerwa ni miongoni mwa wilaya hizo 64 ambazo zinajengewa vyuo vya ufundi stadi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali imekwishapeleka kiasi cha shilingi 324,694,243, pamoja na vifaa vya ujenzi ikiwemo nondo na cement kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kyerwa ambapo ujenzi wa chuo hiki upo katika hatua ya ujenzi wa kuta za boma na ufungaji wa lintel pamoja na ukamilishaji wa misingi, nakushukuru sana.