Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 19 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 256 2024-05-06

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA: aliuliza: -

Je, kuna mpango gani kuhakikisha kila Chuo Kikuu na Vyuo Vishiriki vinashirikiana na halmashauri ili kuwezesha vyuo hivyo kutekeleza umahiri wao?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Vyuo Vikuu na Vyuo Vikuu Vishiriki hushirikiana na Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Majiji katika shughuli mbalimbali kama vile kuendesha semina, warsha na huduma za ugani katika maeneo mbalimbali kulingana na ubobezi wa chuo kikuu husika (outreach activities).

Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile hufanya tafiti ambazo matokeo yake hutumika kutatua changamoto mbalimbali za jamii katika halmashauri husika. Pia kumekuwa na utaratibu wa wanafunzi kutoka vyuo vikuu kufanya mafunzo kwa vitendo katika taasisi zilizopo chini ya halmashauri kwa lengo la kutoa huduma kwa jamii pamoja na kupata uzoefu wa kazi wanazozisomea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, vyuo vikuu vitaendelea kushirikiana kwa karibu na halmashauri zote katika kutoa huduma kwa jamii na kutatua changamoto zinazoikabili jamii. Aidha, naomba mamlaka zote za Serikali za Mitaa kuendelea kutoa fursa kwa taasisi za elimu ya juu kutumia rasilimali zilizopo kuwezesha kutoa mafunzo. Nakushukuru.