Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 48 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 421 2022-06-21

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka umeme katika Vitongoji 503 Wilayani Kyerwa?

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Innocent Seba Bilakwate, Mbunge wa Kyerwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji vyote visivyo na umeme Tanzania Bara kadri ya upatikanaji wa fedha. Aidha, hadi kufikia mwezi Februari, 2022, Serikali imeshapeleka umeme katika Vitongoji 27,934 kati ya vitongoji 64,760. Vitongoji vilivyobaki vitaendelea kupatiwa umeme kupitia miradi ya Ujazilizi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Mradi wa Ujazilizi awamu ya IIB ambao utahusisha pia Mkoa wa Kagera upo katika hatua za ununuzi wa wakandarasi. Katika Mkoa wa Kagera, mradi huu unalenga kusambaza umeme katika vitongoji 126 ambapo kati ya hivyo, vitongoji 34 vipo katika Wilaya ya Kyerwa. Utekelezaji wa mradi huu utaanza mara baada ya hatua za ununuzi wa wakandarasi kukamilika na utafanyika ndani ya miezi 18. Serikali itaendelea kutekeleza miradi ya ujazilizi kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha mpaka hapo vitongoji vyote vitakaposambaziwa umeme. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023, tumeelezea dhamira ya kupeleka umeme kwenye vitongoji vyote nchini na tumetenga kiasi cha shilingi bilioni 140 kwa kuanzia