Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 48 | Finance and Planning | Wizara ya Fedha na Mipango | 428 | 2022-06-21 |
Name
Dr. Florence George Samizi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Muhambwe
Primary Question
MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itakarabati kituo cha Polisi cha wilaya na nyumba za askari katika jimbo la Muhambwe.
Name
Sagini Jumanne Abdallah
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Butiama
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Florence George Samizi Mbunge wa Muhambwe kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uchakavu wa kituo cha Polisi na nyumba nane za makazi ya askari Muhambwe Kibondo. Tathmini ya jumla imeshafanyika na kubaini kuwa kiasi cha shilingi 86,518,500 zinahitajika kwa ajili ya kugharamia ubadilishaji paa, dari, mfumo wa maji safi na maji taka, madirisha na kupaka rangi. Ukarabati huo utafanyika baada ya kupata fedha kulingana na mpango wa Serikali wa ujenzi na ukarabati wa vituo na nyumba za makazi ya askari kuanzia mwaka 2022/2023, nakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved