Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 5 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 62 | 2024-04-08 |
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuanzisha Mradi wa Building a Better Tomorrow katika Bonde la Mto Rufiji?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia Machi, 2024, jumla ya ekari 340,245.3 zimebainishwa na kupimwa afya ya udongo kwa ajili ya Programu ya BBT katika Mikoa ya Dodoma, Kigoma, Mbeya, Singida, Tanga, Njombe na Kagera. Kwa sasa maandalizi ya mashamba yameanza katika Mkoa wa Dodoma.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Wizara imepanga kuanza Mradi wa BBT kwa halmashauri 100 zitakazotenga maeneo yenye hekta 200 kwa kujenga miundombinu ya umwagiliaji na kutoa utaalam. Aidha, halmashauri zitakuwa na jukumu la kudahili vijana kutoka katika halmashauri husika ili waweze kunufaika na programu hiyo. Hivyo, namshauri Mheshimiwa Mbunge ahimize halmashauri yake itenge eneo litakalohitajika ili iwe miongoni mwa halmashauri 100 zitakazonufaika na mpango huo.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved