Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 5 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 63 | 2024-04-08 |
Name
Salim Alaudin Hasham
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ulanga
Primary Question
MHE. SALIM A. HASHAM aliuliza: -
Je, lini Serikali itatoa majibu juu ya umiliki wa Msitu wa Hewa ya Ukaa uliopo Kituti hadi Mgolo?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kifungu cha 23 cha Sheria ya Misitu kimeweka utaratibu wa uanzishaji na usimamizi wa maeneo ya misitu kisheria. Kupitia Tangazo la Serikali Na. 783/2022, Wizara ilikamilisha taratibu za awali za kutoa notisi ya siku 90 za nia ya Serikali ya kuanzisha rasmi Msitu wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga. Kwa sasa Wizara inakamilisha taratibu za kisheria za kuanzisha msitu huo ambao utakuwa chini ya umiliki wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved