Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 26 Finance and Planning Wizara ya Fedha 343 2024-05-15

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. PRISCUS J. TARIMO K.n.y. MHE. SHALLY J. RAYMOND aliuliza:-

Je, mikopo kiasi gani imetolewa na Taasisi za Fedha kwa dhamana ya mali zilizorasimishwa na wanawake wangapi wamenufaika?

Name

Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Magharibi

Answer

WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, benki na taasisi za fedha hutoa mikopo yenye dhamana inayotosheleza (fully secured), yenye dhamana inayotosheleza sehemu tu ya mkopo (partially secured) na isiyo na dhamana (unsecured). Hadi kufikia tarehe 31 Desemba, 2023, zilikuwa zimetoa mikopo yenye jumla ya shilingi bilioni 33,194.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali haina takwimu zinazotenganisha mikopo iliyotolewa kwa wanaume na wanawake. Hata hivyo, Benki kuu ya Tanzania inatengeneza mfumo ambao ukikamilika utaweza kukusanya takwimu zinazotenganisha mikopo iliyotolewa kwa wanaume na wanawake kutoka kwenye benki na taasisi za kifedha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali itaendelea na mchakato wa kuandaa Sheria ya Miamala Salama na Masjala Bayana ya Kielektroniki itakayotumika kusajili dhamana zinazohamishika ili kupanua wigo wa dhamana na hivyo kuwezesha wananchi wengi zaidi kupata mikopo kutoka benki na taasisi za kifedha.